CCM yashinda viti 18 vya udiwani Nyamagana

Muktasari:

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda viti 18 vya udiwani kwenye kata zote za Jimbo la Nyamagana.

Nyamagana. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda viti 18 vya udiwani kwenye kata zote za Jimbo la Nyamagana.

Hayo yamesemwa asubuhi hii ya Alhamisi Oktoba 29, 2020 na Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Kiomoni Kibamba.

Hata  hivyo, Kibamba amesema kazi ya kujumlisha kura za Uraisi na Ubunge inaendelea.

Endelea kufuatilia mitandao yetu ya Mwananchi kwa matokeo zaidi.