CCM yatwaa ubunge na viti vyote vya udiwani Shinyanga

Muktasari:

Mgombea wa CCM,  Patrobas Katambi ametangazwa mshindi kwa kupata kura 31  831 dhidi ya kura 16, 604 alizopata mshindani wake Salome Makamba wa Chadema.

Shinyanga. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda kiti cha ubunge jimbo la Shinyanga mjini pamoja na viti vyote 17 vya udiwani Manispaa ya Shinyanga.

Mgombea wa CCM,  Patrobas Katambi ametangazwa mshindi kwa kupata kura 31  831 dhidi ya kura 16, 604 alizopata mshindani wake Salome Makamba wa Chadema.

Akitangaza matokeo hayo leo Alhamisi Oktoba 29, 2020, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Geoffrey Mwangulumbi amesema Godwin Makomba wa ACT-Wazalendo amepata kura 883 wakati Charles  Shigino wa NCCR-Mageuzi amepata kura 133 huku Abdalla Sube Demokrasia Makini akipata kura 99.

Mgombea Yahaya Khamis wa UDP amepata kura 69 huku  Malengo Elias aliyegombea kwa tiketi ya TLP amevuna kura 63.