CT-Scan Muhimbili yaharibika, wagonjwa wapelekwa Moi na Mloganzila

Muktasari:

  • Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imesema mashine yake ya  CT Scan haifanyi kazi na wagonjwa wa dharura  wanaohitaji huduma hiyo wanapelekwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (Moi) na hospitali ya Mloganzila.

Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imesema mashine yake ya  CT Scan haifanyi kazi na wagonjwa wa dharura  wanaohitaji huduma hiyo wanapelekwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (Moi) na hospitali ya Mloganzila.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Aprili 8, 2020  mkuu wa kitengo cha mawasiliano katika hospitali hiyo,  Aminiel Aligaesha amesema mashine hiyo haifanyi kazi tangu  Aprili 7, 2020, kubainisha kuwa huduma zimesimama katika hospitali hiyo.

“Chanzo ni kuharibika kwa kifaa kinachotoa mionzi ya kupiga picha (CT- scan x-ray tube). Kumekuwa na usumbufu lakini kifaa kilichoharibika tayari kimeagizwa nchini Ujerumani.”