VIDEO: Chadema kuendelea na maandalizi ya mikutano ya hadhara

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kinaendelea na maandalizi ya mikutano ya hadhara ya chama hicho itakayoanza Aprili 4, 2020 kwa sababu maandalizi hayo hayahusishi mikusanyiko ya watu, amesema mkurugenzi wa itikadi, uenezi na mambo ya nje wa Chadema, John Mrema.