Corona ilivyochelewesha ubingwa Simba

Corona ilivyochelewesha ubingwa Simba

Muktasari:

Moja ya tukio kubwa ambalo watu wengi walilimisi kulisoma katika tovuti  ya Mwananchi iliyofungiwa tangu Aprili 16 mwaka huu ni kusimama kwa Ligi Kuu Bara kwa miezi mitatu kutokana na Corona.

Moja ya tukio kubwa ambalo watu wengi walilimisi kulisoma katika tovuti  ya Mwananchi iliyofungiwa tangu Aprili 16 mwaka huu ni kusimama kwa Ligi Kuu Bara kwa miezi mitatu kutokana na Corona.

Msimu huo wa 2019/20 ulimalizika kwa Simba kutwaa ubingwa.

Shirikisho la Soka Tanzanzia (TFF), Machi 17 lilisimamisha ligi zake zote ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali kufuatia mlipuko wa virusi vya Corona duniani kote. Mpaka  Ligi Kuu Bara inasimama wakatu huo timu nyingi zilikuwa zimeshacheza michezo 28 na nyingine 29, Simba ilikuwa kileleni ikiwa na pointi 71.

Hata hivyo Mei 17, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli

alitangaza kuruhusu michezo kurejea baada ya kuona maambukizi ya virusi vya

corona (Covid 19) yanapungua.

"Kama wiki hii tunayoianza kesho hali itaendelea hivi, nimepanga kufungua vyuo ili

wanafunzi wetu waendelee kusoma na pili nimepanga pia sisi kama taifa kuruhusu

michezo iendelee kwa sababu michezo ni sehemu moja ya burudani kwa Watanzania,"

alisema Rais Magufuli wakati  akishiriki Ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT

Usharika wa Chato Mkoani Geita.

Baada ya kauli hiyo ya Rais Magufuli, Ligi Kuu ikarejea Juni 21 na msimu ukamalizika kwa Simba kutwaa ubingwa na kupata nafasi nyingine ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo itaanza baadae mwezi Novemba mwaka huu.

Licha ya Ligi hiyo kuwa na ushindani lakini baadhi ya timu zilionekana kuzidiwa nguvu kutokana na kutokuwa na mazoezi ya pamoja kwa muda mrefu kutokana na mambo mengi kusimama wakati wa Corona.