Corona yaikwamisha Raja kuifuata Zamalek

Muktasari:

Zamalek ilipoteza mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa wa soka barani Afrika ilipofungwa bao 1-0 nyumbani Jumapili iliyopita, na mechi ya marudiano imepangwa kufanyika Jumamosi jijini Cairo, Misri.

Johannesburg, Afrika Kusini (AFP): Klabu ya Raja Casablanca ya Morocco imesema leo kuwa haiwezi kusafiri kwenda Misri kurudiana na Zamalek katika mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika mwishoni mwa wiki hii baada ya wachezaji wake wanane kugundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.

"Mamlaka za Morocco zimefuta kibali kilichotolewa kwa klabu cha kusafiri nje ya nchi," kiongozi mmoja aliiambia AFP. 

Raja, ambayo ilifungwa kwa bao 1-0 nyumbani Jumapili, ilikuwa inatarajiwa kucheza mechi ya marudiano katika Uwanja wa International jijini Cairo Jumamosi.

Wachezaji wanne wa Raja waliokuwa katika kikosi kilichoanza dhidi ya Zamalek Jumapili iliyopita-- beki Ilias Haddad, viungo Omar Arjoune na Mouhcine Moutouali, na mshambuliaji Abdelilah Hafidi -- ni miongoni mwa waliogundulika kuambukizwa ugonjwa wa virusi vya corona, Covid-19.

Vyombo vya habari vya Morocco pia vilimtaja kiungo Abderrahim Achchakir na washambuliaji Anas Jabroun, Ayoub Nanah na Mohamed Zrida kuwa ni miongoni mwa waliopata maambukizi.  

Shangwe zilizoibuka mwezi huu baada ya Raja kutwaa ubingwa wa Morocco kwa mara ya kwanza katika miaka saba, zinahusishwa na maambukizi hayo.