Diamond Platinumz kutumbuiza Ujerumani

Friday September 6 2019

Msanii wa muziki nchini Tanzania, Diamond

Msanii wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz  

By Mwandishi Wetu, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Nyota wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania, Diamond Platnumz kesho Jumamosi Septemba 7, 2019 atafanya onyesho nchini Ujerumani.

Kwa mujibu wa Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Dk Abdallah Possi amesema Diamond atafanya shoo kwenye ukumbi maarufu  Berlin, Columbia Halle.

Amesema atakuwa msanii wa pili kutoka Afrika kufanya onyesho katika ukumbi huo ambao hutumiwa na wasanii maarufu duniani (bila kumtaja msanii wa kwanza alikuwa nani).

“Diamond akiwa na uongozi wake nilikuwa nao leo, nimezungumza nao, na atafanya shoo kesho kwenye ukumbi maarufu Columbia Halle,” amesema Dk Possi.

Kwa mujibu wa ratiba ya ukumbi huo, inaonyesha Diamond atafanya shoo saa 2:00 usiku kwa saa za Ujerumani ambapo hapa nchini itakuwa saa 1:00 usiku.

 

Advertisement

Advertisement