VIDEO: Diamond atumia dakika 20 Jamafest, walinzi na mpiga picha wake wazuiwa

Sunday September 22 2019

 

Msanii wa Muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Diamond Platnumz ametumia dakika ishirini kutoa burudani kwa mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliojitokeza katika Tamasha la utamaduni la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini hapa.

Diamond ametumia dakika 20 kutoa Burudani tofauti na awali ambapo iliripotiwa angetoa burudani kwa dakika 5 pekee.

Katika hatua nyingine walinzi na mpiga picha wa msanii huyo walijikuta katika wakati mgumu na kuzuiwa na maafisa usalama  wakati msanii Diamond alipotakiwa kwenda kumsalimia Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ambaye alikuwa mgeni rasmi.

Advertisement