VIDEO: Dk Bashiru asema uongozi si mali ya kudumu, awaonya wenye viburi

Muktasari:

Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amewataka viongozi mbalimbali nchini Tanzania kuacha kburi kwa kuwa nyadhifa wanazozishika ni za kupita.


Unguja. Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amewataka viongozi mbalimbali nchini Tanzania kuacha kburi kwa kuwa nyadhifa wanazozishika ni za kupita.

Huku akitaja viongozi mbalimbali waliofariki dunia, Dk Bashiru amesema baada ya kufanya mazuri wanakumbukwa kwa mchango wao, kuwataka waliopo sasa kulitambua suala hilo.

Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Novemba 29, 2019 wakati akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Kusini Unguja

“Katibu mkuu, ubunge, uwaziri na urais umeazimwa tu haifai nafasi ya kuazimwa kuitumia kwa kiburi au kudhani ni mali yako ya kudumu.”

“Mzee Karume (Abeid Aman- rais mstaafu wa Zanzibar) aliazimwa hatunaye lakini mchango alioutoa wakati anatumia dhamana hiyo ni wa kudumu. Mwalimu Nyerere (Julius-rais mstaafu wa Tanzania) aliazimwa uhai na afya kwa wakati wake, mchango alioutua ni wa kudumu, yeye hayupo si wa kudumu, wewe na mimi nani,” amesema Dk Bashiru.