Dk Bashiru atamba CCM imefanya kampeni za kistaarabu

Muktasari:

Katibu Mkuu huyo amesisitiza kuwa katika kuelekea kusherehekea ushindi wa chama hicho amani itaendelea kutawala.

Wakati kampeni za uchaguzi Mkuu zikielekea ukingoni Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ali amesema chama chake kimefanya kampeni za kisasa na kistaarabu.

Dk Bashiru amesema licha ya mikutano ya chama hicho kufurika watu wengi haikuwa  ya ghadhabu na hasira bali upendo na furaha vilitawala.

Amesema watanzania wote waliohudhuria mikutano ya CCM wanatambua kuwa mikutano ilikuwa na utulivu mkubwa licha ya kuwa na watu wengi.

Katibu Mkuu huyo amesisitiza kuwa katika kuelekea kusherehekea ushindi wa chama hicho amani itaendelea kutawala.

 “Tujitahidi sana ushindi wa CCM uambatane na kudumisha amani, utulivu na upendo kwa watanzania wote. Uwe chanzo cha kudumisha amani na umoja wa taifa letu.

Tujitokeze Oktoba 28 kupiga kura kwa uhuru na hiari yetu na kuichagua CCM iendelee kubaki madarakani kwa ajili ya kuleta maendeleo kwenye taifa hili,” amesema