VIDEO: Dk Bashiru ayaonya mashirika ya kimataifa kuhusu Tanzania

Thursday November 28 2019

Dk Bashiru, mwananchi habari, gazeti la mwananchi, kisiwani Zanzibar

 

By Muhammed Khamis, Mwananchi [email protected]

Unguja. Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally ameyaonya mashirika ya kimataifa akiyataka kuacha kuingilia mambo ya ndani ya Tanzania.

Dk Bashiru ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Novemba 28, 2019 wakati akizungumza na wajumbe wa chama hicho mkoa wa Magharibi mjini Unguja, Zanzibar.

Amesema ni marufuku ofisi yoyote ya CCM kufanya kazi na taasisi za kimataifa zisizokua na uhusiano na chama hicho.

Dk Bashiru amesema uwepo kwa taasisi za kimataifa nchini Tanzania isiwe sababu ya kuingilia mambo ya ndani ya nchi yasiyowahusu.

Mtendaji mkuu huyo wa CCM  amewaonya mawaziri na watendaji wa chama hicho tawala nchini Tanzania watakaobainika kushirikiana na taasisi za kimataifa kwamba watapoteza kazi.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi

Advertisement


Advertisement