EAC: Hakuna mtumishi aliyeondoka eneo la kazi kwa kutolipwa

Tuesday August 13 2019

By Filbert Rweyemamu,Mwananchi [email protected]

Arusha. Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imesema hakuna wafanyakazi wake yeyote waliondoka katika kituo chake cha kazi kwa sababu ya kutolipwa mshahara.

Hayo yameelezwa leo Jumatano Agosti 13, 2019 na naibu katibu mkuu wa jumuiya hiyo, Stephen Mlote wakati akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Jumuiya hiyo jijini Arusha.

Amesema wafanyakazi 14 akiwemo katibu mkuu, Balozi Liberat Mfumukeko wapo likizo, mmoja yupo likizo ya uzazi na wafanyakazi 11 wapo kwenye shughuli mbalimbali za EAC nje ya Arusha.

" Napenda mfahamu wafanyakazi wote wameshalipwa mishahara yao ya Julai, 2019 kama mnavyofahamu mwaka wa fedha unapoanza sio nchi zote wanachama zinalipa kwa wakati lakini hadi ninavyozungumza nanyi  Uganda pekee ndio imeanza kulipa ada ya mwaka wake wa fedha 2019/2020," amesema Mlote.

Advertisement