Exim yazindua akaunti tatu mpya

Wednesday October 2 2019

By Mwandishi Wetu, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Katika kuboresha huduma zake kwa wateja, Benki ya Exim Tanzania leo Jumatano imezindua huduma mpya zinazolenga kuhamasisha wateja wake na jamii kuhusu uwapo wa akaunti zake mpya tatu zinazofahamika kama akaunti ya ‘Haba na Haba’, ‘Haba na Haba Plus’ na akaunti ya ‘Mzalendo’.

Akaunti zote hizo zinalenga kuwawezesha wateja hao kuhifadhi fedha bila makato ya mwezi kwa matumizi ya kuweka akiba na kwa shughuli za kila siku.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hizo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Amana wa Benki ya Exim Tanzania, Agnes Kaganda alisema huduma hizo zinalenga wateja wote  wakiwamo wenye kipato cha chini, kati na kipato kikubwa.

 

“Akaunti hizi zinalenga kukidhi mahitaji ya wateja ambao wanahitaji kuhifadhi fedha zao kwa matumizi ya siku zijazo. Huduma zote zimelenga kutatua changamoto ya ukosefu wa namna iliyo bora ya kuhifadhi fedha miongoni mwa Watanzania walio wengi bila kuwa na akiba isiyopungua makato ya kila mwezi,’’ alisema.

 

Advertisement

Aidha, akifafanua kuhusu akaunti ya Haba na Haba, Agnes alisema inawalenga watu wenye nia ya kuweka akiba kwa ajili ya malengo ya baadaye huku akitaja faida zinazoambatana na ufunguaji wa akaunti hiyo kuwa ni pamoja na kunufaika na kiwango cha juu cha riba, hakuna makato ya mwezi na huduma ya haraka katika matawi yote ya benki hiyo,

 

 

 

 

Akizungumza kuhusiana na akaunti ya Haba na Haba Plus, Agnes alisema inawalenga watu wenye kipato cha juu ambao pia kupitia akaunti hiyo, wataweza kunufaika na viwango vikubwa vya riba.

 

 Alitaja akaunti ya tatu kuwa ni Mzalendo ambayo itawawezesha wateja kupata huduma ya kufanya miamala ya kila siku kupitia benki hiyo kwa saa 24 na siku saba za wiki bila kukatwa malipo ya kila mwezi  na pamoja na kupatiwa ATM kadi ya malipo bure.

Alizitaja faida za akaunti hiyo kuwa ni pamoja na kutoa fursa kwa mmiliki wake kuweza kuiendesha bila kuwekewa kiwango cha chini cha salio, haina ada ya uendeshaji.

Advertisement