Fedha kutibu malaria zimekwisha- WHO

Muktasari:

Shirika la Afya Duniani limeyataka mataifa wafadhili na Serikali za nchi zinazoathirika na ugonjwa huo kuendeleza mapambano dhidi ya malaria.

Geneva. Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema fedha za kugharamia mapambano dhidi ya malaria na maradhi yanayouwa mtoto mmoja kila baada ya dakika mbili wengi wakitokea Afrika, zimekwisha.

Limesema kwa kuwa mazalia ya mbu ndio chanzo cha malaria, kuna uwezekano ya nusu ya wakazi duniani wakaambukizwa maradhi hayo endapo juhudu za haraka hazitachukuliwa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa (UN) ya mwaka huu, idadi ya watu duniani imefikia bilioni7.7.

Kutokana na hali hiyo, WHO limeyataka mataifa wafadhili na Serikali za nchi zinazoathirika na ugonjwa huo kuendeleza mapambano dhidi ya malaria.

Hata hivyo, mtaalamu wa masuala ya malaria wa shirika hilo, Pedro Alonso anasema idadi ya watu wanaombukizwa ugonjwa huo duniani imepungua.

Mwaka 2017 watu milioni 231 duniani  waliambukizwa malaria na mwaka jana ni watu milioni 228.

Watu 416, 000  walifariki dunia mwaka 2017 huku mwaka jana wakifariki watu 405,000.