Breaking News

VIDEO: Gavana wa Narok, Kenya anusurika kifo ajali ya helikopta

Sunday October 18 2020

Gavana wa jimbo la Narok nchini Kenya, Samuel Tunai, mbunge wa Narok Mashariki, Lemanken Aramat pamoja na watu wengine kadhaa wamenusurika kifo baada ya helikopta waliyokuwa wakisafiria kuanguka muda mfupi baada ya kupaa huko Melili.

Ajali hiyo ilitokea Jumamosi Oktoba 17, 2020 wakati wakitoka katika Kijiji cha Enkipejus kilichopo kaskazini mwa Narok.

Walikuwa wamekwenda kuhudhuria mazishi ya Tompo Ole Sasai, ambaye ni baba wa mkuu wa idara ya fedha wa kaunti hiyo, Julius Sasai.

Shuhuda wa ajali hiyo, Joseph Kamotho amesema awali rubani alijaribu kurusha ndege mara kadhaa lakini haikuwezekana.

"Helikopta hiyo ilifanikiwa kuruka baada ya majaribio kadhaa, kisha ilianguka baada ya kuruka urefu wa mita 100 na ikatoa sauti ya kushangaza."

Ndege hiyo yenye namba za usajili 5Y-MEP ilianguka kwenye shamba la ngano karibu na Kijiji cha Olkipejush na abiria wote walitoka salama.

Advertisement

 

Advertisement