Hazard, Suarez warejea uwanjani leo Hispania, Messi bado

Saturday September 14 2019

Hazard, Suarez warejea uwanjani leo Hispania, Messi bado

 

Madrid, Hispania (AFP).Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema jana Ijumaa kuwa mchezaji aliyenunuliwa kwa bei mbaya msimu huu, Eden Hazard ameruhusiwa na madaktari na hivyo anaweza kupangwa kucheza mechi yake ya kwanza ya lLigi Kuu ya Soka Hiospania leo Jumamosi dhidi ya Levante.

Wakati akisema hayo, Barcelona inategemea mshambuliaji wake wa Uruguay, Luiz Suarez atarejea uwanjaniu leo wakati vigogo hao watakapovaana na Valencia, lakini haitegemei kuanza kumtumia nyota wake, Lionel Messi.

"Wote tunataka kumuona Eden," alisema Zidane. "Kuna shinikizo kubwa juu yake, matarajio makubwa. Lakini yuko tayari na hicho ndicho kitu muhimu sana."

Hazard alikuwa akitarajiw akucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Vigo mwanzoni mwa msimu baada ya kujiunga na vigogo hao wa Hispania akitokea Chelsea mwezi Juni.

Lakini Mbelgiji huyo alipata majeraha akiwa mazoezi ya Chelsea yaliyokuwa yakifanyika Valdebebas na alilazimika kukaa nje kwa wiki tatu, kipindi ambacho real Madrid ilikuwa katika hali ngumu, ikishinda mechi moja na kutoka sare mbili.

Hata hivyo, Zidane ametaka watu kuwa na uvumilivu wakati Hazard akirejea katika hali yake ya kawaida.

Advertisement

"Lazima tuwe wavumilivu," alisemad. "(Hazard) Aliumia kwa wiki tatu am,ekuwa nje na amerejea mazoezini kwa wiki moja.

"Tuna mechi saba katika siku 21 na itatubidi tuzichukulie taratibu. Itakuwa jukumu langu kuangalia kila dakika na muda anaocheza, kwa sababu tunamuhitaji kwa kipindi kirefu, kwa mechiu kadhaa, si moja."

Hazard amerejea katika muda mzuri kwa Madrid ambao wanaanza kampeni ya Ligi ya mabingwa wa Ulaya kwa kuvaana na Paris Saint-Germain wiki ijayo, hasa baada ya kiungo Luka Modric kuumia nyonga.

"Sababu inaanzia sasa," alisema Zidane. "Tuna mechi saba katika siku 21 na nadhani tunahitaji kucheza, kushindana, hicho ndicho wachezaji wanachotaka."

Jijini Barcelona, Suarez anaweza kurejea kwenye kikosi cha Barcelona kitakachovaana na Valencia katika mechi ya Ligi Kuu ya Soka ya Hispania leo Jumamosi, kocha Ernesto Valverde alisema jana Ijumaa, akiongeza kuwa ana matumiani na hali ya Lionel Messi.

"Suarez alishiriki kikamilifu mazoezini jana (Alhamisi) na tena leo," alisema Valverde. "Tunamatiumaini anaweza kucheza."

Mshambuliaji huyo wa Uruguay mwenye umri wa miaka 32 alitoka uwanjani akiwa anachechemea baada ya kupata matatizo ya misuli katika mechi ya kwanza ya vigogo hao msimu huu iliyoisha kwa Athletic Bilbao kushinda kwa bao 1-0.

Alhamisi, Messi, ambaye pia ana tatizo kama hilo, alieleza matumaini kuwa atarejea kwenye kikosi cha Barcelona kabla ya mechi ya Ligi ya mabingwa wa Ulaya dhidi yas Borussia Dortmund Jumanne ijayo.

"Tunadhani amekaribia kurejea uwanjani," alisema Valverde. "Sitaki kusema lolote kuepuka kuweka matarajio makubwa, lakini nadhani itakuwa vigumu kwa Jumanne."

Barcelona imeshjinda mechi moja kati ya tatu ilizocheza La Liga, huu ukiwa ni mwanzo mbaya kuliko yote kwa vigogo hao tangu mwaka 2008.

Msimamo wa La Liga:


Advertisement