Hong Kong yazidi kufukuta, waandamanaji waendelea kushinikiza demokrasia

Muktasari:

Polisi wapambana na waandamanaji usiku kucha na kukamata watu 29.

Hong Kong, China. Polisi visiwani Hong Kong wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakipambamana na askari usiku kucha.

Aidha, watu 29 walikamatwa na polisi wakati wa maandamano hayo yaliyotokea leo Jumapili Agosti 25 katika mji wa Hong Kong.

Awali waandamanaji hao walifunga barabara kwa mawe na kurusha mabomu ya petroli katika eneo la viwanda la Kwun Tong lenye idadi kubwa ya raia wa China Mashariki kwa Kowloon.

Hii ni mara ya kwanza kwa jeshi la polisi visiwani humo kutumia mabomu ya kutoa machozi baada ya kipindi cha wiki moja tangu jeshi hilo lilipowadhibiti waandamanaji katika maneo mbalimbali ikiwamo eneo la uwanja wa ndege.

Waandamanaji wanasema wanakabiliana na kusambaratika kwa mpangilio wa Serikali moja, mifumo miwili unaoipa Hong Kong uhuru wake tangu eneo hilo liliporejeshwa na Uingereza chini ya utawala wa China mwaka 1997.