IGP azungumzia ushirikiano wa polisi wa Tanzania, Burundi

Friday October 11 2019

By Anthony Kayanda, Mwananchi [email protected]

Kigoma.  Ili kupambana na wahalifu wanaovuka mipaka ni lazima kuwe na ushirikiano ya majeshi ya nchi zinazopakana.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa Oktoba 11, 2019 na Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Tanzania (IGP), Simon Sirrokatika kikao  kazi cha viongozi wa Tanzania na Burundi waliokutana mjini Kigoma.

Amesema ni vigumu askari kudhibiti  wahalifu wanaovuka mipaka bila ushirikiano wa nchi  wanakotoka.

"Makosa ya ugaidi, ujangili, dawa za kulevya, ujambazi na biashara haramu ya kusafirisha binadamu huwezi kuishinda ukifanya kazi peke yako.”

“Ni lazima upate ushirikiano kutoka nchi jirani unazopakana nazo. Ndio maana leo tunakutana na wenzetu wa Burundi kujadili na tutasaini mikataba ya ushirikiano baina ya vikosi vyetu vya polisi," amesema Sirro.

Mkuu wa jeshi la polisi Burundi,  Melchiade Ruceke amesema nchi hiyo imeruhusu polisi wake kushirikiana na polisi wa Tanzania kwa ajili ya kupambana na wahalifu wanaovuka mpaka.

Advertisement

"Tutaendelea kuwakamata wahalifu wanaofanya ujambazi Tanzania na kukimbilia Burundi na pia nchi ya Tanzania itawakamata wale wanaoingia kutoka Burundi, tunataka amani katika nchi zetu," amesema Ruceke.

Advertisement