Idadi wanafunzi wa vyuo vikuu yapungua kwa asilimia tano

Thursday June 13 2019

By Sharon Sauwa, Mwananchi [email protected]

Dodoma. Serikali ya Tanzania imesema idadi ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu nchini ilipungua kwa asilimia 4.9 mwaka 2017/18.

Mwaka huo, wanafunzi 230,339 walijiunga vyuo vikuu wakilinganishwa na 242,240 waliodahiliwa mwaka 2016/17 sawa na asilimia 4.9.

“Upungufu huu ulitokana na baadhi ya vyuo  kufungiwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini kutoa programu ambazo zilikuwa hazina wanataaluma wenye uwezo wakufundisha programu hizo,”amesema Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango.

Waziri amesema hayo leo, Juni 13, 2019 alipokuwa anawasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/20.


Advertisement