Kamati ya LAAC yamtaka CAG kufanya ukaguzi halmashauri ya Nyang’wale

Thursday August 22 2019

By Sharon Sauwa, Mwananchi [email protected] mwananchi.co.tz

Dodoma. Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imemwagiza Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalum katika Halmashauri ya Nyang’wale mkoani Geita.

Maagizo hayo yametolewa leo Alhamisi Agosti 22, 2019 na makamu mwenyekiti wa kamati hiyo,  Abdallah Chikota wakati kamati hiyo ilipopitia hesabu za halmashauri hiyo.

Amesema wamebaini ubadhirifu wa fedha za maendeleo katika halmashauri hiyo, kwamba ukaguzi huo utakaofanyika kwa miezi mitatu utabaini ukweli.

“Ukaguzi huu utawezesha walishiriki katika ubadhilifu wa fedha za miradi ambao awali hawakubainika kuchukuliwa hatua pamoja na waliopewa fedha hizi," amesema.

Amesema kamati hiyo maalum itawezesha kufanya ukaguzi wa kina kubaini waliohusika wote na ubadhirifu huo ambao umewakaosesha haki wananchi kunufaika na miradi ya maendeleo


Advertisement

Advertisement