Breaking News

Kampeni zaanza wapinzani wakipinga rais kuendelea

Friday October 16 2020

 

Abidjan, Ivory Coast. Kampeni zimeanza leo nchini Ivory Coast kwa ajili ya uchaguzi wa rais utakaofanyika Oktoba 31, ambao rais aliye madarakani, Alassane Ouattara ameibua utata kwa kutaka kipindi cha tatu huku wapinzani wakishinikiza umma usikubalina kukiwa na dalili za maandamano ya vurugu.

Wachambuzi wanahofia kutopkea tena kwa vurugu kabla au baada ya uchaguzi kama ilivyokuwa mwaka 2010-2011 wakati watu 3,000 walipofariki na taifa hilo la Afrika Magharibi kuingia katika vurugu.

"Wapizani wote wa Ivory Coast wanasema 'hapana, hapana, hapana," kwa Ouattara kupewa kipindi cha tatu, ndio ujumbe uliokuwa unaonyeshwa katika mkutano wa hadhara wa upinzani jijini Abidjan Jumapili uliohudhuriwa na maelfu ya watu.

Kuna wagombea wanne wa urais -- Outarra mwenye miaka 78; rais wa zamani Henri Konan Bedie mwenye miaka 86; na wengine wawili wapya -- aliyekuwa waziri mkuu Pascal Affi N'Guessan na mbunge wa zamani Kouadio Konan Bertin.

Baraza la Katiba liliwakataa watu wengine 40 kugombea urais, akiwemo rais wa zamani Laurent Gbagbo, 75, na kiongozi wa zamani wa waasi, Guillaume Soro, 47, wote wakihusika kwa kiasi kikubwa katika vurugu zilizoikumba nchi hiyo baada ya uchaguzi wa mwaka 2010.

Gbagbo aliachiwa huru kwa masharti na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ya The Hague baada ya kutoonekana na makosa dhidi ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Advertisement

Kwa sasa yuko Brussels akisubiri uamuzi dhidi ya rufaa.

Upinzani unapinga jaribio la Ouattara kuongoza kipindi cha tatu licha ya katiba kumpa rais vipindi viwili tu.

Baada ya kuchaguliwa tena mwaka 2015, Ouattara alitangaza kuwa hangeomba kipindi cha tatu.

Lakini alibadilisha mawazo baada ya mtu ambaye angependa awe mrithi wake, Amadou Gon Coulibaly kufariki kwa shambulio la moyo mwezi Julai.

Advertisement