Kanda ya ziwa yatoa shule kumi bora matokeo darasa la saba

Muktasari:

  • Shule za kanda ya ziwa zang’ara kwenye orodha ya shule 10 bora matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019

Dar es Salaam. Shule za mkoa wa Mara nchini Tanzania umeongoza kwenye matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019 baada ya shule ya Graiyaki kushika nafasi ya kwanza.

Mara haikuishia kutoa shule ya kwanza kwenye kumi bora kwani hata nafasi ya pili katika shule bora ilishikwa na Twibhoki ya mkoani humo.

Nafasi ya tatu imeshikwa na mkoa wa Kagera kupitia shule ya Kemebos.

Mkoa wa Mwanza umeingiza shule nne kwenye orodha hiyo ambazo ni Musabe (5), Tulele (6), Peaceland (8) na Mugini (9).

Kanda ya ziwa bado imeendelea kutesa kwenye shule 10 bora ambapo mkoa wa Shinyanga nao uliingiza shule tatu kwenye orodha hiyo ambazo ni Little Treasures (4), Kwema Modern (7) na dimba likafungwa na Rocken Hill.