Katavi-Rukwa yazidi kuunganishwa kwa lami

Wednesday October 9 2019

By Mary Clemence, Mwananchi [email protected]

Katavi. Rais wa Tanzania,  John Magufuli amemuagiza  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack  Kamwelwe kufanya upembuzi yakinifu ili kipande cha barabara ya Sitalike- Kibaoni mkoani Katavi chenye urefu wa kilomita 71 kujengwa kwa kiwango cha lami.

Kiongozi mkuu huyo wa nchi ametoa agizo hilo leo Jumatano Oktoba 9, 2019 wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Mlele katika mkutano hadhara uliofanyika kijiji cha Kibaoni.

Amesema Mkoa wa Katavi ni kati ya mikoa inayozalisha mazao mengi ya chakula na biashara, hivyo ni lazima barabara hiyo ijengwe kwa kiwango cha lami kuwasaidia wakulima kusafirisha mazao yao.

Magufuli leo alifungua barabara ya Kanazi-Kizi na Kibaoni inayounganisha mkoa wa Katavi na Rukwa yenye urefu wa kilomita 76.6 iliyojengwa  kwa kiwango cha lami kwa Sh100.5bilioni

 

 

Advertisement

Advertisement