Kigoma, Kagera na Geita kupata umeme wa uhakika

Tuesday February 25 2020

 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Mikoa ya Kigoma, Kagera na Geita itaanza kunufaika na nishati ya umeme kuanzia Novemba 2020 baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo kikubwa cha kupoza umeme unaotoka Gridi ya Taifa ya Geita mpaka Nyakanazi.

Kukamilika kwake kutafanya uzalishaji wa nishati hiyo kufikia megawati 72 kutoka megawati 22 za sasa.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani alipotembelea mradi wa Nyakanazi na kueleza umeme huo utakaokuwa mkubwa zaidi ya uliopo sasa utaongezeka zaidi hadi megawati 200 baadaye, kuwataka makandarasi kumaliza kazi yao Novemba 2020 badala ya Januari 2021.

Kalemani amewakaribisha wawekezaji wa viwanda kuanza matayarisho kwa kuwa umeme utakuwa wa uhakika.

Kalemani amesema manufaa mengine ya mradi huo ni wakati reli ya kisasa (SGR) itakapofika Kigoma, kwamba itatumia umeme huo kwa sababu uliopo ni mdogo.


Advertisement

Advertisement