Kikwete: Tanzania ya sasa sio niliyoiacha

Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete

Muktasari:

Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema haoni uwezekano wa CCM  kushindwa kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, 2020 kwa kuwa chama hicho kimefanya mambo makubwa.

Dar es Salaam. Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema haoni uwezekano wa CCM  kushindwa kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, 2020 kwa kuwa chama hicho kimefanya mambo makubwa.

Amesema Tanzania ilivyo leo sio ilivyokuwa mwaka 2015 wakati anang’atuka madarakani, akibainisha kuwa kwa sasa imepiga hatua kubwa ya maendeleo.

Akizungumza jana Jumatatu  Oktoba 19, 2020 kwenye mkutano wa kampeni wilayani Bagamoyo, Kikwete amesema chama hicho kimefanya makubwa hivyo watanzania watashukuru kwa kukipigia kura.

“Sina wasiwasi utashinda sana na chama chetu kitashinda na kuendelea kuongoza Taifa. Sioni hofu ya mgombea wetu kushindwa wala CCM kushindwa.”

“Sioni sababu ya hilo kwa sababu chama chetu chini ya uongozi kimeiongoza vizuri nchi yetu.

Mambo mengi mazuri yamefanyika, wananchi wanatambua na wataonyesha shukrani yao Oktoba 28 kwenye sanduku la kura,” amesema.