VIDEO: Kinana, Lowassa wamuombea kura Magufuli

VIDEO: Kinana, Lowassa wamuombea kura Magufuli

Muktasari:

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana amesema Magufuli ametekeleza ahadi zake alizotoa wakati wa ziara zake mikoani; na amekuja na ahadi mpya zenye zaidi ya kurasa 300 kwa ajili ya kuwahudumia Watanzania

Dar es Salaam. Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana ameungana na makada wengine wa chama hicho akiwemo Edrward Lowassa kumuombea kura mgombea urais, John Magufuli.

Akizungumza wakati wa mkutano wa kampeni Jimbo la Arusha Mjini Kinana amesema kuna sababu nne za kumpa miaka mitano mingine Magufuli.

“Nataka niungane na Watanzania wenzangu kumuombea kura Magufuli amefanya kazi kubwa nne ya kwanza ametekeleza ilani kama alivyoahidi, ametekeleza ahadi zake wakati anafanya kampeni, ametekeleza ahadi zake alizotoa wakati wa ziara zake mikoani;  na amekuja na ahadi mpya zenye zaidi ya kurasa 300 kwa ajili ya kuwahudumia Watanzania,”amesema..

Kwa upande wake Lowassa amewakata Watanzania kufanya uamuzi sahihi wasiingie kwenye machafuko.

 “Leo Venezuela kuna fujo, Nigeria kuna fujo kwa sababu ya mambo ambayo sisi yanatuletea Amani. Rais wetu amekuja na ndoto sahihi kabisa amejitahidi na wananchi wameelewa sasa tumpe zawadi ya kura kwa mazuri aliyofanya,” amesema Lowasa akimalizia kuimba wimbo aliokuwa akiimba Magufuli wakati wa kampeni za mwaka 2015.

Hata hivyo, Magufuli aliwahoji maelfu ya watu waliofurika uwanjani hapo, “Mmemuona mzee Lowassa kapendeza eeh CCM nzuri mshangilieni.”