Kocha Liverpool akana kuwafokea wachezaji wake dhidi ya Salzburg

Muktasari:

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amedai hakuwa na hasira dhidi ya wachezaji wake baada ya timu yake kutanguliwa kufungwa mabao matatu jana usiku.


London, England. Kocha wa Liverpoo, Jurgen Klopp amesema hakuna  hasira dhidi ya wachezaji wake licha ya kuzidiwa na Salzburg.

Klopp alisema hakuridhika na kiwango cha wachezaji wake hasa dakika 45  za kipindi cha kwanza.

Liverpool iliongoza kwa kufunga mabao 3-0 kipindi cha kwanza kabla ya Salzburg kusawazisha, lakini mabingwa watetezi Liverpool walifanikiwa kuibuka na ushindi wa 4-3 katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Klopp aliwatolea maneno makali baadhi ya wachezaji kwa kufanya uzembe na kutoa nafasi kwa wapinzani wao kusawazisha mabao matatu ndani ya saa moja.

Dakika ya 69 ilikuwa nzuri zaidi kwa kocha huyo wa zamani wa Borussia Dortmund baada ya Mohamed Salah kufunga bao la ushindi.

Safu ya ulinzi Liverpool ilionekana kuyumba na kutoa nafasi kwa Salzburg  kukaribia lango lao mara kwa mara.

“Tulipoteza umakini na upepo ulibadilika Salzburg ilipopata bao la kwanza. Sikuwa na hasira au jambo jingine lolote lile, niliona wachezaji wakirejea mchezoni na kucheza kwa kiwango bora,” alisema Klopp.