Kolabo ya wasanii Aslay, Ali Kiba yakata kiu ya mashabiki

Thursday September 5 2019

 

By Rhobi Chacha, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, Ali Kiba na Aslay wamekata kiu ya mashabiki  ikiwa ni mara yao ya kwanza kuachia wimbo wa pamoja.

Wimbo huo uitwao ‘Bembea’ uliotolewa jana Jumatano Septemba 4, 20189 umeendelea kufanya vizuri katika mtandao wa Youtube.

Hadi kufikia leo mchana takribani watu 503,293 walikuwa wameutazama wimbo huo ndani ya saa 22 tangu uwekwe kwenye mtandao huo, huku ukiwa unaongoza namba moja.

Kwenye ukurasa wa Instagram wa Ali kiba kumekuwa na mgawanyiko wa maoni kutoka kwa watazamaji wa video ya wimbo huo ambapo wengi walikuwa wanapongeza na wachache kuuponda.

Ali Kiba aliandika kwa kifupi chini ya video ya wimbo huo “Msimu wa hits unafunguliwa na Bembea – Mchukue wa ubani wako, mpenzi wako, mwandani wako halafu bembea nae mahabani.

Ujumbe uliofuatiwa na maoni ya mashabiki hao.

Advertisement

Bonifas Mwitah" Jamani Raha hichi ndio kitu nilikuwa nakisubiria sana toka mwanzoni hello timu kiba pita na hii."

 

Lazaro Nkanga "Yaani Aslay na King Kiba mmetuchelewesha kutupa kitu roho inapenda mashabiki zenu yaani hiki ndio nilikuwa nataka kifanyike siku zote"

Michael_alphonce “Hii nyimbo mbaya bwana, mnaisifia kinafiki.

Faidha Hamisi "Kitu cha motooo kabisa yaani hapa Kiba huku dogo Aslay huhuu yaani mmenipa raha mpaka naona kama nabembea"

craizy_lion “bro #alikiba kubali tu, ushafeli kimuziki, badala ya kwenda mbele wewe unarudi nyuma.

Hawa Bilali "Vijana niwapendao nimefurahi kuwaona pamoja hapa hakuna kilichobadilika safi sana"

ezma_milers23 “Simbaa sio mda anachafua hali ya hewaa..

Advertisement