Lissu: Nichagueni kuwa rais niwe mfariji wenu

Muktasari:

Mgombea urais kupitia Chadema, Tundu Lissu amewaomba Watanzania kumchagua ili aweze kuwafariji kwa kuwatatulia kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili, ikiwemo ukosefu wa maji safi na salama.

Dodoma. Mgombea urais kupitia Chadema, Tundu Lissu amewaomba Watanzania kumchagua ili aweze kuwafariji kwa kuwatatulia kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili, ikiwemo ukosefu wa maji safi na salama.

Lissu ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Oktoba 17, 2020 katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa barafu.

Amesema akiwa rais atahakikisha anakuwa mfariji kwa kusimamia maslahi ya watumishi ambao hawajapata nyongeza ya mishahara kwa kipindi cha miaka mitano, na  wanaokabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama, akitolea mfano wilaya ya Chato mkoani Geita.

"Nimefika maeneo yote ya Tanzania nimesikia changamoto nyingi, mfano wilaya ya Chato wananchi wanakabiliwa sana na tatizo la maji, wameuzidi hata mkoa wetu wa Singida. Ukienda shuleni kuna upungufu wa madarasa wanafunzi wamejaza, nipeni dhamani niwe mfariji wenu," amasema Lisu.

Amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi Septemba 28, 2020 kupiga kura kwani ni haki yao ya kikatiba.