Lyon yashindwa kuipiku PSG kileleni Ufaransa

Saturday September 14 2019

Paris, Ufaransa (AFP).Lyon jana Ijumaa ilipoteza nafasi ya kushika usukani wa Ligi Kuu ya Soka Ufaransa ilipolazimishwa sare ya mabao 2-2 na Amiens licha ya kupata mabao mawili yaliyofungwa na Moussa Dembele.

Mchezaji wa Amiens, Mathieu Bodmer alisawazisha katika dakika ya mwisho na kuwapa wenyeji pointi moja.

Lyon inayofundishwa na Sylvinho sasa imefanikiwa kukusanya pointi mbili tu katika mechi zake tatu zilizopita na inaendelea kuwa nyuma ya Paris Saint Germain kwa tofauti ya pointi moja kabla ya mabingwa hao wa soka wa Ufaransa kuvaana na Strasbourg leo Jumamosi.

Lyon, ambao walikuwa wakichukuliwa kuwa ndio wapinzani wakubwa wa PSG katika mbio za ubingwa mwanzoni mwa msimu, watavaana na vigogo hao wanaofundishwa na Thomas Tuchel mwishoni mwa wiki ijayo.

"Wakati unapokuwa huchezi dakika 90, unaadhibiwa," alisema Sylvinho, ambaye timu yake inakutana na Zenit Saint Petersburg katika mechi ya Ligi ya Mabingwa wa Ulkaya Jumanne.

Waliruhusu bao la kwanza dakika saba tu baada ya mchezo kuanza wakati beki mkongwe wa Lyon, Christophe Jallet kuuacha mpira kutoak kushoto kujaa wavuni.

Advertisement

Lakini Dembele aliendeleza mwanzo mzuri msimu huu alipofunga kwa kiki ya juu na kiusawazisha dakika mbili tu baadaye.

Mchezaji huyo wa zamani wa Celtic mwenye umri wa miaka 23 alipiga tik-tak kuugeuzia wavuni mpira wa krosi kutoka kwa Bertrand Traore katikia dakika ya 34, akifunga bao lake la tano la ligi msimu huu.

Martin Terrier alinyimwa bao la tatu la Lyon mwanzoni mwa kipindi cha pili kutokana na umahiri wa kipa Regis Gurtner, na Lyon wakalazimika kuruhusu bao la kusawazisha katika dakika za majeruhi.

Mapema jana, mchezaji chipukizi wa Nigeria, Victor Osimhen pia alifunga bao lake la tano msimu huu wakati Lille ilipopata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Angers.

Osimhen, mwenye miaka 20, alifunga bao la kwanza dakika sita kabla ya mapumziko na sasa analingana na Dembele katika orodha ya wanaoongoza kwa ufungaji katika ligi hiyo ya Ufaransa.

Msimamo wa Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1)

Paris SG                                4 3 0 1 10  2 9

Rennes                 4 3 0 1  6  3 9

Lille                                        5 3 0 2  7  5 9

Nice                                       4 1 0 1  7  5 9

Angers                  5 3 0 2  9  9 9

Lyon                                      5 2 2 1 12  4 8

Reims                    4 2 1 1  4  1 7

Nantes                 4 2 1 1  4  3 7

Marseille                             4 2 1 1  3  3 7

Toulouse                             4 2 1 1  4  5 7

Bordeaux                            4 1 2 1  5  5 4

Brest                     4 1 2 1  3  5 5

Nimes                   4 1 1 2  6  7 4

Montpellier        4 1 1 2  2  3 4

Metz                     4 1 1 2  4  6 4

Amiens                 5 1 1 3  5  8 4

Saint-Etienne     4 1 1 2  3  6 4

Strasbourg          4 0 3 1  3  5 3

Monaco                               4 0 2 2  2 10 2

Dijon                     4 0 0 4  1  7 0


Advertisement