Maajabu tuzo za Grammy, wasanii maarufu wakosekana tuzo kubwa

Muktasari:

Tuzo za Grammy ni moja ya matamasha makubwa ulimwenguni ya muziki ambayo hutuza wasanii waliofanya vizuri kwa mwaka.


Orodha ya mwisho ya wanamuziki watakaowania tuzo katika Tamasha la 62 la Grammy, ambalo hutuza wasanii waliofanya vizuri, inajumuisha wanamuziki wanaochipukia na kuwaengua waliokuwa wanategemewa kung'ara.

Mashabiki wanasikitikia kutokuwepo kwa wanamuziki kadhaa wapya na wa zamani, ikijumuisha wachache waliozoeleka watakaopata tuzo katika tamasha hilo litakalofanyika Januari 26, 2020 katika ukumbi wa Stapple Center.

Katika wanamuziki nyota ambao wanakosekana katika baadhi ya tuzo muhimu ni pamoja na Taylor Swift ambaye ametajwa kuwania tuzo tatu tu, na mara moja tu katika tuzo kubwa, akiwa ametoa albamu yake ya saba ya "Lover" ambayo imetajwa kuwania tuzo ya Albamu Bora ya Mwaka.

Wengi pia walitarajia bendi maarufu ya wavulana ya BTS kuteka tamasha la mwaka 2020, lakini walisahaulika kabisa kwa wapigaji kura wa Grammy.

Bruce Springsteen, ambaye ameshatwaa tuzo 20, pia ameshindwa kuingia katika orodha ya wanaowania tuzo licha ya albamu aliyotoa peke yake ya "Western Stars," na filamu yake ya "Springsteen on Broadway" inayotamba katika mtandao wa Netflix haijatajwa katika kipengele cha Filamu Bora ya Muziki.

Wanamuziki wa miondoko ya pop, Ed Sheeran na The Jonas Brothers hawakuwa na kikubwa cha kutambia baada ya kila mmoja kutajwa katika kipengele kimoja.

Wabashiri wengi walitegemea Chance the Rapper angalau kutajwa katika tuzo ya Albamu ya Mwaka kama si Albamu Bora ya Rap, lakini msanii huyo ameingiza wimbo katika kipengele cha Wimbo Bora wa Rap.

Malkia wa muziki wa pop pia ameachwa: Madonna, ambaye ametwaa tuzo za Grammy mara saba akiwa ametajwa mara 28, hakutajwa katika tuzo licha ya kutoa albamu yake ya 14 ya Madame X.

 

- Walioshangaza -

Walioshangaza katika orodha ya wanaowania tuzo ni Bon Iver na wasanii wa rock, Vampire Weekend.

Rapa Lil Nas X aliruka hadi kileleni mwa orodha hiyo baada ya kutajwa kuwania tuzo sita, akiongoza wimbi la mafanikio ya rap ya nchi yao kwa albamu ya "Old Town Road" iliyopata mafanikio ya haraka.

Mashabiki walitarajia msanii huyo mwenye umri wa miaka 20 atangazwe kuwania tuzo za Msanii Mpya Bora na Rekodi ya Mwaka, lakini ametajwa zaidi.

Marapa wawili ambao walitumia muda wao mahabusu nchini Marekani, wametajwa kuwania tuzo ya Albamu Bora ya Rap: Meek Mill na 21 Savage wote walikabiliana na vita tata vya kisheria zilizotokana na tuhuma za ubaguzi.

21 Savage alikamatwa akiwa kwao Atlanta na maofisa wa idara ya uhamiaji ambao walisema alikuwa anaishi Marekani kinyume cha sheria baada ya visa yake kuisha muda mwaka 2006, wakati akiwa mdogo -- na katika kile kilichosahangaza mashabiki wake ni kubaini kuwa alizaliwa Uingereza.

Mill alikuwa na tatizo la ubaguzi wa rangi lakini alilimaliza mwaka huu.