Maalim Seif aeleza kwanini Lissu

Mwenyekiti wa chama cha ACT- Wazalendo, Maalim Seif Shariff Hamad 

Muktasari:

Mwenyekiti wa chama cha ACT- Wazalendo, Maalim Seif Shariff Hamad  amewataka Watanzania kumpigia kura mgombea urais kupitia Chadema, Tundu Lissu kwa madai kuwa ndio mwenye uwezo wa kumshinda mgombea wa CCM, John Magufuli.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa chama cha ACT- Wazalendo, Maalim Seif Shariff Hamad  amewataka Watanzania kumpigia kura mgombea urais kupitia Chadema, Tundu Lissu kwa madai kuwa ndio mwenye uwezo wa kumshinda mgombea wa CCM, John Magufuli.

Ameeleza hayo leo Jumanne Oktoba 20, 2020 kwenye uwanja wa Barafu Mburahati wakati akiwanadi wagombea ubunge na udiwani wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema wakati wa mkutano Mkuu wa chama hicho walikubaliana kumuunga mkono mgombea mmoja wa upinzani mwenye nguvu baada ya kuona kampeni za mgombea wa chama hicho, Bernard Membe zinasuasua.

"Kamati ya uongozi ya ACT ambayo niliiongoza mimi mwenyewe na Membe akiwepo tulikubaliana tumuunge mkono Tundu Lissu" amesema Seif.

Seif ambaye pia ni mgombea urais Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo amesema wakati huu ni wakati wa kufanya mabadiliko na mtu pekee mwenye uwezo wa kuleta mabadiliko ni Lissu