Maalim Seif kuwania uongozi ACT-Wazalendo

Muktasari:

Mshauri mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania, Maalim Seif Sharif Hamad kesho Alhamisi Januari 30, 2020 atachukua fomu  ya kugombea uongozi wa chama hicho.

Dar es Salaam. Mshauri mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania, Maalim Seif Sharif Hamad kesho Alhamisi Januari 30, 2020 atachukua fomu  ya kugombea uongozi wa chama hicho.

Maalim Seif anachukua fomu hiyo siku mbili baada ya chama hicho kufungua pazia la uchaguzi wa viongozi wake wakuu

baada ya kukamilisha uchaguzi wa viongozi wa ngazi za chini.

Kwa mujibu wa ratiba, uchukuaji fomu kuwania nafasi mbalimbali umeanza Januari 27 na utamaliza Februari 26, 2020.

Taarifa ya chama hicho inaeleza kuwa, Maalim Seif atachukua fomu hizo kesho saa 5 asubuhi.

Kabla ya kujiunga na ACT, Maalim Seif alikuwa katibu mkuu wa CUF ambako aliondoka baada ya kuibuka mgogoro ndani ya chama hicho.