Magufuli: Wenye viwanda angalieni bei zenu za mabomba

Monday September 16 2019

 

By Bakari Kiango, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli amewaeleza wamiliki wa viwanda vya mabomba nchini kuwa Serikali inapotaka kuwalinda lazima na wao waangalie namna biashara inavyokwenda.

Mkuu huyo wa nchi ameeleza suala hilo, akiwa na maana kuwa wamiliki hao waangalie na suala la bei la bidhaa hiyo kama wanataka iwalinde.

Rais Magufulia ametoa kauli leo Jumatatu Septemba 10, 2019 wakati akizundua Kiwanda cha  kutengeneza mabomba cha Pipe Indrustries Limited kilichopo Vingunguti.

 “Wenye viwanda angalieni suala la bei zenu. Inawezekana bei za mabomba yenu ni ghali kuliko yanayotoka nje ya nchi. Naambiwa wakati mwingine bei za mabomba nchini zipo juu kuliko yanayoagizwa kutoka nje. Bomba linatoka nje linalipiwa kodi lakini  bado linakuwa na gharama nafuu kuliko lililotengenezwa hapa Vingunguti,”amesema Rais Magufuli.

Amewaambia kuwa Serikali inapotaka kuwalinda lazima waangalia suala hilo, kwa kuwa biashara ni ushindani huku akiwataka kufanya uchambuzi kuhusu ubora na bei za  mabomba  hayo.

Amesema jambo jema tayari Serikali imeshaweka utaratibu mzuri kwenye malighafi zinazoagiwa kwa ajili ya kuwarahisishia katika uzalishaji. 

Advertisement

“Angalieni ubora wa mabomba mnayozalisha, kizuri chajiuza kibaya chajitembeza, tengenezeni bidhaa zinazokubalika,” amesema Rais Magufuli.

Advertisement