Magufuli aagiza bosi TPDC kurejeshwa kazini haraka

Monday July 22 2019

 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli ameiagiza Wizara ya Nishati kumrejesha kazini mara moja aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dk James Mataragio.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Julai 22, 2019 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ya Tanzania imesema, Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo kwa kuitaka Wizara ya Nishati kumrejesha Dk Mataragio katika nafasi yake ya Mkurugenzi Mkuu wa TPDC ili aendelee na majukumu yake.

Taarifa hiyo imesema Dk Mataragio alisimamishwa kazi na Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC, Agosti 20 mwaka  2016.

Tangu Dk Mataragio aliposimamishwa, nafasi yake ilikuwa ikikaimiwa na Kapuulya Musomba.

Advertisement