Magufuli ataja sababu za kuliita soko jina la Ndugai

Friday November 22 2019

 

By Sharon Sauwa, Mwananchi [email protected]

Dodoma. Rais John Magufuli amesema miongoni mwasababu zilizofanya soko la Nzuguni kulipa jina la Ndugai ( Spika la Bunge Job Ndugai) ni kitendo chake cha kuruhusu azimio la Dodoma kuwa makao makuu ya Serikali kujadiliwa bungeni.

Akizungumza na wananchi leo Ijumaa Novemba 22 2019, Rais Magufuli amesema Ndugai angeweza kukataa azimio lisiingie Bungeni.

"Hata mimi nafanana naye kwa kulipa jina lake itabaki kwenye historia," amesema Rais Magufuli.

Akizungumzia miradi ya maendeleo,  Rais Magufuli amesema uwanja  wa Msalato utajengwa kwa gharama ya  Sh 500bilioni.

Amewataka wakazi wa Dodoma pia wasiwe na hofu ya upatikanaji wa maji kwasababu maji ya bwawa la Farkwa yanatosha kwa matumizi ya Wilaya ya Dodoma na maeneo ya majirani.

Advertisement