Breaking News

Magufuli kuendelea na kampeni Pwani, kuhitimisha Dodoma

Saturday October 17 2020

By Pamela Chilongola, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Mgombea urais kupitia CCM, John Magufuli Oktoba 19, 2020 ataendelea na mikutano ya kampeni katika mikoa sita akianzia Pwani na kumalizia mkoani Dodoma Oktoba 26, 2020.

Wakati Magufuli akichanja mbuga katika mikoa hiyo, mgombea mwenza, Samia Suluhu Hassan ataendelea na mikutano Zanzibar na Kassim Majaliwa ambaye ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM atakuwa Mtwara na Lindi.

Hayo yameelezwa leo Jumamosi Oktoba 17, 2020 na katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole  katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Amesema mbali na mkoa wa Pwani, Magufuli ataendelea na kampeni katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara na kumalizia Dodoma.

Amesema Samia ataelekea Zanzibar na kuhitimisha mkoani Morogoro na Majaliwa mikoa ya Kusini ikiwa ni pamoja na Lindi na Mtwara.

Advertisement