Mahakama yakataa DC Chemba kumtaliki mkewe

Muktasari:

Odunga na Mbuwuli wanadaiwa kufunga ndoa ya Kikristu katika Kanisa la Sabato Sinza Dar es Salaam mwaka 2000 na kupata cheti cha ndoa  A no 00140917.

Dar es Salaam. Mahakama ya Mwanzo Ukonga imekataa ombi la mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga kumpa talaka mkewe, Medilina Mbuwuli  na kuamuru atoe Sh7 milioni kama nusu ya gharama za matunzo aliyotumia mkewe kumsomesha mtoto wao kuanzia darasa la kwanza hadi sasa pamoja na Sh100,000 za matunzo kila mwezi.