Majeruhi wawili ajali ya moto Morogoro wafariki, idadi yafikia 99

Tuesday August 20 2019

Majeruhi,  ajali moto Morogoro, wafariki, mwananchi habari, yafikia 99

 

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro (RC) nchini Tanzania, Dk Stephen Kebwe amesema vifo vinavyotokana na ajali ya lori la mafuta ya petroli kuanguka kisha kuwaka moto imefikia 99 baada ya majeruhi wawili kufariki dunia.

Majeruhi hao waliofariki ni kati ya 18 waliokuwa wamelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam katika chumba cha uangalizi maalum (ICU).

Akizungumza na Mwananchi kwa simu leo jioni Jumanne Agosti 20,2019, Dk Kebwe amesema, “Kwa taarifa ambazo tumezipata kutoka Muhimbili hadi leo saa 10 jioni, majeruhi wawili kati ya 18 wamefariki dunia na kufikisha idadi ya vifo 99.”

“Kwa maana hiyo kwa sasa kuna majeruhi 16 huku Morogoro na 16 Muhimbili wakiendelea na matibabu,” ameongeza mkuu huyo wa mkoa.

Ajali hiyo ya lori ilitokea asubuhi ya Jumamosi Agosti 10, 2019 eneo la Msamvu mkoani Morogoro baada ya kuanguka kisha kulipuka.

Soma zaidi

Advertisement

Advertisement