Majeruhi wengine wawili ajali ya moto Morogoro wafariki, idadi yafikia 97

Monday August 19 2019

ajali ya lori, mafuta ya petroli,Itingi Msamvu,Taifa Muhimbili,ICU,

 

By Elizabeth Edward, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Majeruhi wawili kati ya 20 wa ajali ya lori la mafuta ya petroli lililoanguka kisha kuwaka moto waliokuwa wamelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam nchini Tanzania wamefariki dunia.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano MNH, Aminiel Aligaesha akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Agosti 19,2019 amesema majeruhi waliobaki hospitalini hapo ni 18 ambao wote wapo kwenye chumba cha uangalizi maalum (ICU).

Amewataja waliofariki ni Rosijo Mollel (35) aliyefariki jana Jumapili mchana na Neema Chakachaka ambaye amefariki alfajiri ya leo Jumatatu.

Vifo hivyo viwili, vinafikisha idadi ya waliofariki kutokana na ajali hiyo kufikia 97.

 

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi

Advertisement


Advertisement