Makamu wa Rais Zimbambwe ametoweka

Tuesday August 20 2019

 

Zimbambwe. Makamu wa Rais wa zamani wa Zimbabwe, Phelekezela Mphoko ametoweka polisi baada Tume ya Kupambana na Rushwa ya Zimbabwe (ZACC) kutangaza kumuhoji.

Kiongozi huyo ambaye alitakiwa kujisalimisha katika taasisi hiyo kuhusiana na madai ya rushwa anadaiwa kuondoka wakati gari lake lilipowakaribia maafisa wa taasisi hiyo.

Kiongozi huyo alikuwa makamu wa Rais chini ya Robert Mugabe kabla ya kung’olewa madarakani na jeshi la nchi hiyo mwaka 2017.

Wakili wa kiongozi huyo, Zibusiso Ncube alisema mteja wake alitoweka baada ya kuhofia kukamatwa na kuwekewa sumu.

Wakili Ncube alisema mteja wake alikuwa tayari kujibu maswali lakini aliondoka aliposikia polisi walikuwa na maagizo ya kumtia kizuizini.

Kiongozi huyo pia alihudumu pamoja na Rais wa sasa Emmerson Mnangagwa.

Advertisement

Inaelezwa kuwa Mphoko alikuwa sehemu ya kikundi ambacho kilitaka Neema ambaye ni mke wa Rais Mugabe afanikiwe badala ya Mnangagwa.

Gazeti la Guardian la Zimbambwe limeripoti kuwa tume hiyo ya rushwa ilitaka kumuhoji kiongozi huyo juu ya madai ya unyanyasaji wa ofisi.


Advertisement