Makonda aomba wadada wa Kinyarwanda wawe wengi Jamafest, Waziri wao amjibu

Sunday September 22 2019
pic makonda

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam nchini Tanzania, Paul Makonda amemuomba Waziri wa Utamaduni wa Rwanda, Esparance Nyirasafari kuhakikisha anawaleta wadada wengi kuliko wanaume wa nchi hiyo katika Tamasha lijalo la Utamaduni la Afrika Mashariki (Jamafest).

Makonda  ameta ombi hilo leo Jumapili Septemba 22, 2019 katika uzinduzi wa tamasha hilo uliofanywa na Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Amesema amefuatilia katika mitandao wadada hao wamekuwa wakifuatiliwa kuliko mataifa mengine na kuongeza endapo watakuja wengi ana imani vijana wengi watahamasika kufika kuangalia tamasha hilo lililoanza jana Jumamosi na kuhitimishwa Septemba 28, 2019.

"Waziri nikuombe tu kitu katika tamasha jingine wadada hawa wa Kinyarwanda uwalete wengi kuliko wakina kaka kwani wanafuatiliwa zaidi kuliko wanaume wao," amesema Makonda huku  shangwe zikiibuka kutoka kwa wahudhuriaji wa tamasha hilo

Mwananchi ilimtafuta Waziri Nyirasafari ili kusikia majimbu ya ombi la Makonda ambapo amesema  wamelipokea ombi na kueleza hata mwaka 2019 wanawake walioshiriki sio wachache.

"Jumla ya Wanyarwanda waliokuja hapa ni 107 kati yao 60 ni wanawake hivyo ninaona idadi yao bado ni kubwa ukilinganisha na wanaume,” amesema

Advertisement

"Lakini niseme nimepokea ombi la Mkuu huyo wa Mkoa hivyo watarajie kuona idadi ya wanawake ikiongezeka katika tamasha lijalo ambalo pia litafanyika Tanzania," amesema

Katika hatua nyingine, Makonda amesema anafurahi Mkoa huo kuendelea kuandaa matukio makubwa na hiyo inachangiwa na kuwepo kwa amani katika mkoa huo.

Pia amesema kufayika Jamafest linaongeza nguvu ya kiuchumi katika mkoa huo na mshikamano.

Advertisement