Makonda awatangazia neema mabalozi, wenyeviti wa mashina

Saturday October 05 2019
picc makonda

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameahidi kutoa Sh100 milioni kwa ajili ya kuanzisha mfuko wa kuweka na kukopa mabalozi na wenyeviti wa mashina wa CCM.

Makonda amesema hayo leo Jumamosi Oktoba 15,2019 alipokuwa akisoma  utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa mwaka 2015 /2019 katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Katika mkutano huo uliofanyika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, mkuu huyo wa mkoa amewasilisha utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Makonda amesema fedha hizo zitawasaidia mabalozi wa nyumba kumi na wenyeviti wa mashina kujikimu kiuchumi kwa kukopeshana na kurejesha.

“Fedha hizi natoa ili wasiendelee kuteseka, zitawasaidia kufanya maendeleo,” amesema Makonda.

Awali, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salam, Sylvia Katekamba alisema mkutano huo wa kikatiba umefanyika uwanjani kwa sababu hakukua na ukumbi unaomudu idadi ya wajumbe wa mkutano huo.

Advertisement

“ Kwa hiyo leo tunapokea ilani, tunapokea kazi iliyofanywa na Serikali ya mkoa wa Dar es Salaam,” amesema Katekamba.

Advertisement