Mama atuhumiwa kumchinja, kumla mwanaye

Muktasari:

  • Mkazi wa kijiji cha Mavanga, wilayani Ludewa mkoani Njombe, Christina Mlelwa (38) anashikiliwa na Polisi akituhumiwa kumchinja mwanae, Joseph Bumbilo ambaye ni mlemavu wa viungo kisha kumpika na kumla nyama.

Dar es Salaam. Mkazi wa kijiji cha Mavanga, wilayani Ludewa mkoani Njombe, Christina Mlelwa (38) anashikiliwa na Polisi akituhumiwa kumchinja mwanae, Joseph Bumbilo ambaye ni mlemavu wa viungo kisha kumpika na kumla nyama.

Mume wa mwanamke huyo, Daniel Bumbilo alieleza juzi kuwa mkewe aliwahi kujaribu kufanya tukio kama hilo miaka ya nyuma kwa mtoto wao mwingine anayesoma.

Alisema wakati huo majirani walifanikiwa kumdhibiti na kumnusuru mtoto huyo.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka, alifika eneo la tukio na kuagiza polisi kutafuta ukweli wa tukio hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Khamis Issa alisema wanaendelea na uchunguzi ili wahusika wachukuliwe hatua stahiki.

Katika mahojiano na polisi inadaiwa mwanamke huyo ambaye ana matatizo ya akili alikiri kutenda tukio hilo na kwamba viungo vingine alivitupa porini na chooni.

Kamati ya ulinzi na usalama mkoani Njombe ilipokwenda kwenye pori kunapodaiwa kutupwa baadhi ya viungo hivyo na kuvikuta.