VIDEO: Mamia ya waombolezaji washiriki ibada mazishi ya Mengi

Muktasari:

Reginald Mengi, mwenyekiti wa kampuni za IPP alifariki dunia usiku wa kuamkia Mei 2, 2019 Dubai, Falme za Kiarabu

Moshi. Mamia ya waombolezaji leo Alhamisi Mei 9, 2019 wamejitokeza katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Moshi Mjini kushiriki ibada ya mazishi ya aliyekuwa mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi.

Baadhi ya waliofika kanisani hapo ni mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, mbunge wa kuteuliwa, Anne Kilango  na mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuongoza ujumbe wa Serikali katika mazishi ya Mengi aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Mei 2, 2019 Dubai, Falme za Kiarabu.

Viongozi wengine wanaotarajiwa kushiriki ibada hiyo ni Spika Job Ndugai na katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally.