Mashirika 13 ya ndege yahamia jengo la Terminal III

Muktasari:

  • Mashirika 13 ya ndege zinazofanya safari zake nje ya Tanzania  yamehamishia ofisi zake katika jengo la tatu la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (NJIA) kutoka jengo la pili la uwanja huo. Jengo la tatu linatumiwa na ndege zinazofanya safari zake nje ya nchi hiyo

Dar es Salaam. Mashirika 13 ya ndege zinazofanya safari zake nje ya Tanzania yamehamishia ofisi zake katika jengo la tatu la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (NJIA).

Kabla ya jengo la tatu kuanza kutumika, ofisi za kampuni hizo zilikuwa katika jengo la pili la uwanja huo.

Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Julius Ndyamukama amesema hadi juzi Agosti 19, 2019  mashirika matatu yanayofanya safari za kimataifa yalikuwa bado hayajahamia katika jengo hilo jipya.

 “Kuhamia ni mchakato na shirika linahama mchakato unapokamilika,” amesema Ndyamukama.

Mashirika yaliyokuwa bado yapo jengo la pili la uwanja huo hadi juzi ni Air Mauritius, KLM/Delta na Precision Air huku Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) likiwa  katika majengo yote mawili.

Mashirika yanayotumia jengo la tatu ni Air Mozambique, Air Zimbabwe, Egypt Air,  Fly Emirates, Ethiopia Airlines, Kenya Airways,  Malawian Airlines, Oman Air,  Quatar Airways, Swiss Air, South African Airways, Turkish Airlines,