Matokeo ya awali uchaguzi ni mchuano wa CCM na Chadema

Muktasari:

Matokeo ya awali ya ubunge katika vituo mbalimbali nchini Tanzania yanaonyesha mpambano ni kati ya CCM na Chadema.

Dar es Salaam. Matokeo ya awali ya ubunge katika vituo mbalimbali nchini Tanzania yanaonyesha kuwapo kwa  mpambano   kati ya CCM na Chadema.

Wananchi kote nchini walipiga kura kuanzia leo asubuhi Jumatano kuchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano, wabunge, wawakilishi na madiwani.

Pamoja na uchaguzi kuhusisha vyama 19, CCM na Chadema ndio wanaonekana kuchuana vikali.

Kwa matokeo ya awali ya  jimbo la Dodoma Mjini, mgombea wa CCM, Anthony Mavunde alikuwa anaongoza katika kituo cha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, akiwa na kura 84, akifuatiwa na Aisha Madoga Chademà aliyepata kura 23.

Pia katika kituo cha ofisi ya zamani ya mkuu wa mkoa, Mavunde aliongoza kwa kura 72, akifuatiwa na Madoga wa Chadema aliyepata kura 26.

Katika jimbo la Mwanga mkoani Kilimanjaro, mgombea wa CCM, Anania Tadayo amepata kura 109 akifuatiwa na Kileo Henry wa Chadema (24).

Wagombea wengine ni pamoja na Ummy Salum Mchomvu wa CUF aliyepata kura moja, Joyce Edwin Mfinanga wa NCCR Mageuzi na Godfrey Mwanga wa TLP ambao hawakupata hata kura moja.

Matokeo ya awali jimbo la Same Magharibi kituo cha  Idara ya Kazi Mathayo David wa CCM kura 69,  Gervas Mghonja wa Chadema kura 38.

Katika kituo cha  CWT namba 3, kata ya Mwanga Kaskazini jimbo la Kigoma mjini, Kilumbe Ng'enda CCM  kura 75 na Zitto Kabwe ACT-Wazalendo kura 60 huku Mangu Francis wa Chadema kura mbili.

Jimbo la Ubungo kituo cha Shule ya sekondari mashujaa

Mashujaa A4, Kitila Mkumbo wa CCM kura 137 na

Boniface Jacob wa Chadema kura  30, huku kituo cha Mashujaa B kitila akiwa na kura 84 na Jaco kura 40. Kituo cha Mashujaa B3, Kitila amepata kura 88 na Jacob kura 41.