Matumizi ya R na L yawachanganya wapinzani uchaguzi serikali za mitaa

Muktasari:

Viongozi wa Chadema mkoani mara wameeleza kuwa baadhi ya makosa yaliyowaengua wagombea wao katika kinyanganyiro cha uchaguzi wa serikali za mitaa ni matumizi ya herufi R na L katika ujazaji wa fomu

Dar/ Mikoani. Wakati Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo akitoa maagizo kwa wagombea walioenguliwa kwenye kinyanganyiro cha uchaguzi wa Serikali za mitaa warejeshwe kama walienguliwa kimakosa baadhi ya makosa mbalimbali yaliyowakosesha nafasi ya kugombea yameanza kutajwa.

Mkoani Mara, baadhi ya wagombea kwa mujibu wa katibu wa Chadema mkoani humo, Heche Chacha wanadaiwa kuenguliwa kwa makosa ya kisarufi kwa kuandika neno ‘wiraya’ badala ya wilaya huku wengine wakiwemo wenyeviti waliomaliza muda wao wakidaiwa kuwa sio raia au kukosea mipaka ya maeneo wanayoishi.

Miongoni mwa maeneo yaliyotajwa na Heche kuongoza kwa wagombea kuenguliwa ni yale wanayotoka viongozi wa kitaifa wa serikali, CCM na Chadema ikiwemo kata za Binagikata, Gwintirio na Itirio.

Kwa habari zaidi soma gazeti la Mwananchi la leo Jumatano Novemba 6, 2019