Mbowe ashindwa uchaguzi wa ubunge jimbo la Hai

Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Freeman Mbowe

Kilimanjaro. Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema amekuwa kiongozi na mbunge wa zamani wa kwanza wa chama hicho kushindwa kutetea nafasi yake ya ubunge baada ya mshindani wake kutangazwa kuwa mshindi jimbo la Hai.

Mgombea Sashisha Mafue wa CCM ametangazwa mshindi kwa kupata kura 89, 786 dhidi ya kura 27, 684 alizopata Mbowe aliyekuwa akitetea kiti cha jimbo hilo.

Mbaruku Mhina wa ACT-Wazalendo amepata amepata kura 315.

Matokeo hayo yametangazwa na msimamizi wa uchaguzi jimbo la Hai, Yohana Elisha saa 9:00 alfajiri ya Oktoba 29, 2020.

                                                                                      

Taarifa zaidi kukujia endelea kufuatilia Mwananchi