VIDEO: Mbowe kugombea uenyekiti Chadema

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (kulia) akirejesha fomu za kuwania uenyekiti wa chama hicho kwa katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa leo Jumamosi Novemba 30, 2019. Picha na Filbert Rweyemamu

Muktasari:

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe leo Jumamosi  Novemba 30, 2019 amerejesha fomu ya kuwania uenyekiti wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania.

 


Arusha. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe leo Jumamosi  Novemba 30, 2019 amerejesha fomu ya kuwania uenyekiti wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania.

Amerejesha fomu hizo katika mkutano wa uchaguzi wa viongozi wa chama hicho Kanda ya Kaskazini unaofanyika jijini Arusha.

Mbowe alichukuliwa fomu hiyo na wanachama waliochanga Sh1 milioni kulipia gharama na kumkabidhi. Baada ya kuipokea mbunge huyo wa Hai aliikabidhi kwa katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa.

Mara baada ya kukabidhi fomu hiyo, wanachama waliofurika katika ukumbi unakofanyika mkutano huo walishangilia na wengi walisikika wakisema, “Mbowe tano tena tuvushe.”

Katika uchaguzi huo upinzani mkali upo kati ya mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na mbunge wa Rombo, Joseph Selasini wanaowania uenyekiti wa Kanda ya Kaskazini.